MAELFU ya wananchi wa mkoa wa Mara pamoja na mikoa jirani wakiongozwa na viongozi wa Serikali,Dini na vyama vya Siasa wameuaga mwili wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara John Gabriel Tupa aliyefariki juzi asubuhi akiwa wilayaniTarime kwa shughuli za kikazi.
Akitoa salamu za rambirambi za Serikali mkoani Mara,Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Mara Bartazal Kichinda alisema walipokea kwa masikitiko makubwa msiba wa ghafla wa mkuu wa mkoa wa Mara John Gabriel Tupa kwa kuwa msiba huo umekuja wakati mchango na usaidizi wa kiongozi huyo ukiwa unahitajika zaidi mkoani Mara.