
PICHA mpya ya ‘video queen’ matata Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange’ na mwanaume mmoja ambaye jina lake halikutambulika mara moja, imezua utata kutokana na ukaribu wao.
Picha hiyo ilitupiwa katika mitandao ya kijamii mwishoni mwa wiki iliyopita huku ikisindikizwa na maneno kuwa wawili hao ni wapendanao hali iliyosababisha wadau wengi kupongeza kuwa ni kapo nzuri.