Bunge la Kenya lakubali ndoa ya wake wengi....Mwanaume anaruhusiwa kuoa wanawake hata 10, tena bila mashauriano yoyote na mke wake

No Comments


Bunge nchini  Kenya limepitisha sheria inayomruhusu mwanaume kuoa wake wengi atakavyo, na halazimiki kumshauri mke wake juu ya uamuzi huo.

Katika marekebisho ya Sheria ya Ndoa ya Kenya yaliyopitishwa Alhamisi iliyopita,ndoa zote zitatakiwa kusajiliwa na umri wa chini  wa mwanamke kuweza kuolewa umewekwa ili kuzuia ndoa za mapema  za watoto, hasa wasichana.

Siku hiyo ya Alhamisi Wabunge wote wanaume, ambao ni wengi, waliunga mkono kuondolewa kwa kipengele katika Sheria hiyo ya Ndoa kilichomtaka mwanaume afanye mashauriano na mkewe kwanza kabla ya kuoa mwanamke mwingine.

Wabunge wanawake walilaani hatua hiyo,  walikuja juu na kususia kikao kwa kutoka nje wakidai Sheria hiyo haiwatendei haki wanawake
back to top