
1.0 UTANGULIZI
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilianzishwa kwa sheria Na. 9 ya mwaka 2004 na kuanza rasmi majukumu yake Julai 2005. Bodi ina majukumu makuu mawili; kwanza ni kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu kwa ajili ya masomo ya Shahada au Stashahada ya juu.
Jukumu la pili ni kukusanya marejesho ya mikopo iliyotolewa kwa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu tangu mwaka 1994.
2.0 UTOAJI WA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Tangu kuanzishwa kwake, Bodi imefanikiwa kutoa mikopo kwa idadi kubwa ya Wanafunzi ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla Bodi haijaanzishwa. Mwaka 2005/2006 Bodi ilipoanza kazi ilitoa mikopo kwa Wanafunzi 42,729 wa elimu ya juu kwa kutumia bajeti shilingi Bilioni 56.1.
Idadi ya Wanafunzi wa elimu ya juu wanaopewa mikopo imeendelea kuongezeka kutoka wanafunzi 42,729 mwaka 2005/2006 hadi Wanafunzi 97,348 mwaka 2012/2013. Hii ni sawa na ongezeko la wastani wa 10.4% kwa mwaka. Mikopo iliyotolewa kwa Wanafunzi wahitaji iliongezeka kutoka TZS 56.1 Bilioni mwaka 2005/2006 hadi TZS 306 Bilioni mwaka wa fedha 2012/2013.
Kwa mwaka wa masomo 2013/2014, jumla ya wanafunzi 95,178 wamenufaika na mikopo hadi kufikia tarehe 15 Machi, 2014 ambao mikopo ya kiasi cha TZS 223,977,042,853.00 imekwishalipwa.
Mwaka
|
Idadi ya Wanafunzi Waliokopeshwa
|
Ongezeko
(%)
|
Kiasi kilichoko-peshwa
(Tshs Bilioni)
|
Ongezeko
(%)
|
2004/05 (Na Wizara)
|
16,345
|
-
|
9.9
|
-
|
2005/2006
|
42,729
|
161.4
|
56.1
|
467
|
2006/2007
|
47,554
|
11.3
|
76.1
|
35.7
|
2007/2008
|
55,687
|
17.1
|
110.8
|
45.6
|
2008/2009
|
58,798
|
5.6
|
139.0
|
25.5
|
2009/2010
|
72,035
|
18.4
|
237.8
|
28.7
|
2010/2011
|
92,791
|
28.8
|
230.0
|
24.5
|
2011/2012
|
94,533
|
2.0
|
311
|
35.0
|
2012/2013
|
97,348
|
2.9
|
335.2
|
7.2
|