African Magic Viewers' Choice Awards kutolewa leo (March 8) jijini Lagos Nigeria, Siri ya Mtungi inawania vipengele 7

No Comments

  



Moja kati ya tuzo kubwa zenye heshima Afrika zinazojulikana kama African Magic Viewers’ Choice Awards zinazoandaliwa na Multichoice Africa na Amstel Malta zitafanyika leo (March 8) jijini Lagos Nigeria na kuwakutanisha vinara wa filamu barani Africa.
 
Tamthilia maarufu ya Tanzania ‘Siri ya Mtungi’ inawania tuzo hizo katika vipengele 7 ambavyo ni muigizaji bora kwenye drama wakiwakilishwa na Juma Rajab Rashid (2A), Best Television Series Comedy/Drama, Best Indigenous Language (Swahili), Best Art Director (Kyle Quint), Best Sound Editor (Jordan Riber), Best Costume Designer (Doreen Estazia Noni) na Best Make Up artist (Rehema Samo).
 
Waigizaji wa Siri Ya Mtungi watakaohudhuria tuzo hizo, watakuwa na waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr. Fenella Mukangara.
 
Katika kuchagua washindi wa tuzo hizo, washindi katika vipengele 9 kati ya vipengele 27 vinavyoshindaniwa watachaguliwa moja kwa moja na watazamani kwa kupiga kura kwa SMS au kupitia tovuti maalum ambayo ni www.amvcaawards.dstv.com na washindi wengine katika vipengele 18 watachaguliwa na jopo la majaji.
 
Tuzo hizo zitapambwa na burudani kali toka kwa mkali wa Skelewu, Davido, weningi ni Flavour, Kakadu na Waje huku jukwaa likipambwa na shangwe za host wa siku hiyo IK na Vimbai Mutinihri wa Big Brother Africa.
 
Watazamaji wanaweza kuangalia utoaji wa tuzo hizo kupitia DStv; Africa Magic Entertatainment (Channel 150/151), AfricaMagic (Channel 154) na AfricaMagic World (DStv channel 155)

back to top