
Habari wapendwa, natumai nyote ni wazima wa afya na manaendelea kupambana il kulijenga taifa letu.
Ningependa kwa kifupi mawazo au nguvu iliyonisukuma nianzishe Pamoja blog(pamojasisi.blogspot.com) na pamoja fan page (twitter na facebook)...
Ndoto yangu kubwa ni kuona sisi kama vijana wa Tanzania na ulimwengu kwa ujumla tunasimama kwa miguu yetu wenyewe na kuleta maendeleo na mabadiliko katika nyanja mbalimbali..
"usisubiri uletewe mabadiliko, mabadiliko ni mimi na wewe"
Barack Obama

Nilifikiri haya katika uanzilishaji wa Pamoja
Ndoto yangu kubwa ni kuona sisi kama vijana wa Tanzania na ulimwengu kwa ujumla tunasimama kwa miguu yetu wenyewe na kuleta maendeleo na mabadiliko katika nyanja mbalimbali..
"usisubiri uletewe mabadiliko, mabadiliko ni mimi na wewe"
Barack Obama

Nilifikiri haya katika uanzilishaji wa Pamoja
- Ni fursa zipi za kimaendeleo ambazo zipo
- Ni kwa nini vijana/watu wengi hawafanikiwi
- Je ni ndoto zipi ambazo vijana tunazo na uhalisia wake katika jamii
- Ni vitu gani vijana na jamii kwa ujumla tunahitaji n kuvipenda
- Ni kipi kifanyike ili tufike kwenye kilele cha mafanikio
- Vijana kama muhimili wa taifa
Kujua fursa zilizopo katika ulimwengu tulionao ni hatua muhimu sana katika kupanga ni kipi kifanyike
ili kuzitumia nafasi hizo kwa utoshelevu(maximum) ili kuleta ustawi bora na maendeleo katika jamii yetu...
Kujua na kutambua ndoto zako, ni hatua ya msingi sana katika kuleta ustawi binafsi wa fikra na mwisho
matunda katika jamii. kuwa na ndoto hujenga msingi na ari ya kufanya jambo fulani kwa imani kuwa katika
mawazo yetu ipo siri kubwa sana ya mafanikio la msingi ni kujua uhalisia wa ndoto zako za maendeleo katika jamii.
"Jifunze kuwa karibu na sauti iliyomo ndani yako"
Kutambua mawazo yapi vijana na jamii kwa ujumla wanayapenda ni hatua muhimu sana katika kuleta ustawi
na maendeleo kwani hujenga ufanisi na ari zaidi ya kufanya jambo husika, iliwahi kusemwa
"Kipaji toka moyon" Zantel na "mafanikio huja kwa kupenda unachofanya" Farid Kubanda(Fid Q)
Wengi hukata tamaa na kuvunjika moyo kwa kushindwa kutambua ni kipi wafanye ili waweze kufanikiwa.
Kimsingi zipo njia nyingi za mafanikio ila kuchagua ipi ya kufata ni mtihani kwa kila mmoja, hivyo wana Pamoja tusichoke kushirikishana mawazo na njia zipi tufate ili tufanikiwe.
"Vijana ni Taifa la leo na sasa"..
kimsingi sisi kama vijana tuna dhamana ya maendeleo ya taifa letu, hivyo wakati tulionao ni mwafaka kabisa
katika kuleta mabadiliko ndani ya jamii yetu...
"fikiri zaidi"
Ipo siri katika kutumia akili na uwezo wetu binafsi katika kuibua mawazo, nafasi na chachu za maendeleo.
usichoke kufikiri ni kipi utafanya ili kuleta mabadiliko na mafanikio katika jamii zetu
"Akili inachowaza, akili huweza kufanya"
usikate tamaa. jipe moyo.....Pamoja tutafika...
Ni mtazamo wangu, tushirikishane mawazo zaidi katika hili,,
Nawapenda...
