MFANYABIASHARA WA MAGARI ANASWA AKITAKA KUMLAWITI MODO MAARUFU


EEH Mungu! Unaweza kukataa lakini ni ukweli kwamba dunia imekwisha! Mambo yanayotendeka kila kukicha juu ya ardhi yanathibitisha hilo.
mfanyabiashara wa magari (kushoto) chumbani akitaka kumlawiti modo maarufu.
Mfanyabiashara maarufu wa magari jijini Dar es Salaam aliyefahamika kwa jina la Juvenali amekumbwa na aibu ya mwaka baada ya kunaswa mtupu chumbani na mmoja wa wabunifu wa mavazi ‘modo’ maarufu Bongo (jina tunalihifadhi kwa sasa kwa sababu za kimaadili).
...amefungwa pingu.
Tukio hilo la aibu lilimkuta mfanyabiashara huyo nyumbani kwake, Mbezi ya Tangi-Bovu jijini Dar es Salaam hivi karibuni ambapo wawili hao walinaswa chumbani wakiwa watupu katika mtego maalum.

KISA KILIPOANZIA
Chanzo cha kufichuka kwa taarifa hizo ni modo huyo kumwonesha kaka yake (naye jina tunalo) meseji ‘tamutamu’ kutoka kwa mfanyabiashara huyo kwenda kwake akimshawishi kumlawiti.

KAKA MTU ACHARUKA
Ilidaiwa kuwa kaka mtu alikasirika, aliamini kitendo cha mfanyabiashara huyo kutaka kumlawiti mdogo wake ni kuidhalilisha familia.
“Kaka akamwambia mdogo wake kwamba ni lazima wamtege jamaa huyo ili kumshikisha adabu na ache tabia hiyo,” kilisema chanzo.
                                               .Akitaitiwa na Polisi
                      ...Mfanyabiashara  huyo akichukuliwa na polisi.

                                             ...Safari ya kuelekea kituo cha polisi cha Kawe.
KATIKA ENEO LA TUKIO
Fasta, askari hao walielekea Mbezi Tangi - Bovu, kituo cha daladala eneo la mtego ambapo mfanyabiashara huyo alimuahidi kijana huyo akamchukulie hapo kwenda naye kwenye nyumba ya kumfanyia usodoma.

MFANYABIASHARA AFIKA NA GARI
Wakiwa mita kadhaa, polisi, walimuona mfanyabiashara huyo akiwasili na gari aina ya GX 100 (namba za usajili tunazo). Alifunga breki miguuni kwa kijana huyo, akamfungulia mlango, naye akazama ndani.
Safari ilianza kuelekea upande wa Bagamoyo lakini mita chache gari hilo lilikata kulia.  maafande walikuwa wakifuatilia kwa nyuma bila kujulikana.
                                       ...Akiwa kituo cha polisi.
GARI LAFIKA NYUMBA YA TUKIO
Baada ya mwendo wa kama kilometa mbili, gari hilo lilifika kwenye nyumba  moja na kupiga honi kisha geti  likafunguliwa, gari likaingia na geti likafungwa.

SHETANI ATUPIWA ZIGO
Maafande walimuuliza ‘biznesmani’ huyo ni kwa nini wamekutwa uchi tena wanaume watupu chumbani, alijibu kuwa walikuwa wanahisi joto ndiyo maana waliamua kuvua nguo zote.

Lakini akaongeza: “Jamani niacheni. Hii ni aibu, nitawapeni chochote kile mnachotaka, shetani ndiye alinipitia jamani.”

SAFARI KUELEKEA LUPANGO
Mfanyabiashara huyo alichukuliwa na askari hao hadi polisi lakini baadaye akahamishiwa Kituo cha Kawe ambako shauri hilo liliandikishwa na kupewa jalada la kesi namba KW/RB/1747/2014.
Baada ya kuchukuliwa maelezo, mfanyabiashara huyo aliswekwa lupango akisubiri sheria kuchukua mkondo wake.
back to top